Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Maboresho ya Kodi

Umuhimu wa maboresho ya kodi katika ukuaji soko la hisa

21st Feb, 2025


MABORESHO ya kodi ni jambo muhimu katika kubadili hali ya uchumi kwa kuwa yanagusa moja kwa moja sekta mbalimbali, likiwamo soko la hisa. Nchini Tanzania, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ndilo jukwaa kuu ambapo maboresho haya ya kodi yanadhihirika. Kwa mujibu wa maoni yaliyokusanywa na gazeti la DailyNews kutoka kwa wataalamu wa soko la hisa, maboresho ya sera za kodi yanaweza kuathiri imani ya wawekezaji, kiasi cha biashara na kuathiri soko lenyewe kwa namna mbalimbali. Yafuatayo ni maoni yaliyotolewa na watalaamu hao kuhusu suala hili pamoja na maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili kuunda mfumo bora wa kodi kwa ukuaji endelevu wa nchi. Meneja wa Utafiti na Uchambuzi wa Vertex International Securities, Beatus Mlingi anasema, “Kwa kiasi kikubwa maboresho ya kodi huathiri uamuzi katika uwekezaji, huathiri mzunguko wa mtaji na pia, huathiri shughuli za soko.”

Read More