Wasifu
Balozi Mwanaidi Maajar
MjumbeNi Wakili wa masuala ya sheria na taratibu za biashara na uwekezaji. Ni mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya mawakili REX Attorneys. Alikuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uingereza na Marekani. Ni Mwenyekiti Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kampuni nyingine binafsi na ni mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Wanasheria Wanawake -TAWLA. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika sekta binafsi na ya Umma.
