Wasifu
Balozi Maimuna Tarishi
MjumbeNi Katibu Mkuu Mstaafu aliyebobea katika Utawala wa Umma na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo. Mratibu wa Maboresho ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na Ugatuaji wa Madaraka kwa Umma (D by D). Amehudumu kama Katibu Mkuu katika Ofisi na Wizara mbalimbali, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Geneva na Vienna. Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Ana uzoefu wa Utumishi wa Umma wa zaidi ya miaka 38.
