Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Maboresho ya Kodi

Wasifu

Prof. Florence D. Luoga
Prof. Florence D. Luoga
Mjumbe

Ni Profesa Mshiriki mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mbobezi wa sheria za kodi, sheria za kiuchumi (economic laws) na biashara za kimataifa. Pia ni Gavana mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania. Amehudumu kama Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania (GBT), Wakili mwandamizi wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa Tanzania, na mshauri wa kisheria katika masuala mbalimbali katika utumishi wa umma. Amehudumu katika Utumishi Umma kwa zaidi ya miaka 37.