Wasifu
CPA. Abubakar M. Abubakar
MjumbeNi mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) na pia amewahi kuwa mjumbe wa Bodi ya Chemba ya Biashara ya Zanzibar (ZNCC) ni mbobezi wa masuala ya kodi, ukaguzi wa hesabu na utawala wa fedha anayehudumu kama Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Zanzibar (Zanzibar University), mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 wa mifumo ya Kodi, ukaguzi wa mahesabu na utawala wa fedha akiwa amehudumu pia Benki Kuu ya Tanzania kama mkaguzi wa ndani.
