Wasifu
Balozi Ombeni Yohana Sefue
MwenyekitiNi Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, na Mwanadiplomasia nguli aliyebobea pia katika masuala ya Utawala wa Umma na Sera.
Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 47 katika Utumishi wa Umma na amehudumu kama Katibu Mkuu Kiongozi; Balozi na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa; Balozi nchini Marekani na Mwakilishi Nchini Mexico; Balozi nchini Canada na Mwakilishi Nchini Cuba; Mwandishi wa Hotuba na Msaidizi wa Marais wa Awamu ya Pili na ya Tatu. Kwa miaka mitano (5) alikuwa Mjumbe wa Jopo la Watu Mashuhuri wa Kutathimini Utawala Bora Barani Afrika (APRM), na pia amekuwa Mwenyekiti wa Bodi na Tume mbalimbali.
